explain-icon

Ufafanuzi

Haepukani mwanadamu na kukosea, kwa jinsi alivyoumbwa kutokana na udhaifu, na kutokumtii msimamizi wake katika kutekeleza yale aliyomtaka ayafanye, na kuacha yale aliyomkataza, lakini yeye Mtukufu amefungua mlango wa toba kwa waja wake, na akaeleza kuwa mbora wa wakosefu ni wale wenye kukithirisha toba.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Katika mambo ya mwanadamu ni kukosea na kuingia katika dhambi. La msingi kwa muumini atakapojiiingiza katika maasi afanye haraka kuleta toba.