Alisimama Mtume rehema na amani ziwe juu yake akihutubia kwa Maswahaba zake kwa sentensi tano kamilifu, nazo ni: Ya kwanza: Kuwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka halali. Ya pili: Haiwezekani katika haki yake kulala; kulingana na ukamilifu wa usimamizi wake na uhai wake. Ya tatu: Ya kwamba Yeye Mtukufu anashusha mizani na kuinyanyua kulingana na vile vinavyopimwa miongoni mwa matendo ya waja yanayopanda kwake juu, na zinapimwa riziki zao zinazoshuka katika Ardhi, riziki ambayo ndiyo sehemu na fungu la kila kiumbe huishusha Yeye Mtukufu na kumfanya awe masikini, na huipandisha na kumfanya awe tajiri. Ya nne: Hupandishwa kwake waliyoyafanya waja usiku kabla ya mchana unaofuata baada yake, na amali zao za mchana kabla ya amali za usiku unaofuata baada yake; Malaika wanaohifadhi matendo ya waja hupanda na matendo ya usiku baada ya kumalizika kwake katika mwanzo wa mchana, na wanapanda na amali za mchana baada ya kumalizika kwake katika mwanzo wa usiku. Ya tano: Pazia lake Mtukufu linalozuia kumuona ni nuru au moto, laiti angelifunua basi mwangaza wa uso wake ungeunguza kila kitu mpaka pale linapoishia jicho lake katika viumbe vyake; mwangaza wa uso wake ni nuru yake na utukufu wake na mng'ao wake. Na makadirio: Nikuwa, lau angeliondoa na kukifunua kinachozuia kumuona ambacho ni pazia, na akajitokeza wazi nuru ya uso wake ingeliunguza kila kitu mpaka linapoishia jicho lake katika viumbe vyake; navyo ni viumbe vyote; kwa sababu jicho lake Aliyetakasika na kutukuka limezingira viumbe vyote.