Anatahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutokuendelea kubaki katika dhulma kwa kufanya maasi na ushirikina na kuwadhulumu watu haki zao, kwani Allah Mtukufu humpa muda dhalimu na humchelewesha na humpa umri mrefu na mali nyingi hamharakishii adhabu; ikiwa hatotubia basi humchukua mara moja na huwa hambakishi na huwa hamuachi kwa sababbu ya wingi wa dhulma zake. Kisha akasoma -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Na hivyo ndivyo kuadhibu kwa Mola wako Mlezi anapoikamata miji inapokuwa imedhulumu. Hakika adhabu yake ni chungu na ni kali" [Hud:102]