Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-akasema: @Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mimi sijaacha dhambi yoyote wala maasi yoyote madogo wala makubwa isipokuwa nimeyafanya, je mimi nitakuwa ni mwenye kusamehewa? Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema kumwambia: Hivi wewe hautamki neno la shahada "Ash-hadu an-laa ilaha illa llahu wa anna Muhamadan rasuulullah? Akarudia kumwambia hivyo mara tatu, Basi akajibu: Ndiyo nashuhudia, Basi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akampa habari ya ubora na utukufu wa shahada mbili na namna inavyofuta makosa, na kuwa toba hufuta makosa yaliyopita.