explain-icon

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa wakikutana waislamu wawili kwa mapanga yao, akiwa na dhamira kila mmoja wao ya kummaliza mwenzake; Basi muuaji motoni kwa sababu ya kutekeleza mauaji ya kumuua mwenzake, Kuhusu muuliwaji, hilo likamtatiza Swahaba: Ni vipi anakuwa motoni? Akaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa hata yeye pia anakuwa motoni kwa sababu ya pupa yake ya kumuua mwenzake, na hakikumzuia kuuwa zaidi ya muuaji kumuwahi na kummaliza.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Anastahiki adhabu mwenye kukusudia madhambi kwa moyo wake na akazifanya sababu zake.
  • Tahadhari kali ya kutopigana waislamu kwa waislamu, na kuna ahadi ya moto.
  • Mapigano kati ya waislam kwa haki hayaingii katika ahadi hii ya adhabu, mfano kama kuwapiga vita waasi na mafisadi.
  • Mwenye kutenda dhambi kubwa hakufuru kwa kulifanya pekee; Kwa sababu Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kawaita wenye kupigana kuwa ni waislamu.
  • Watakapokutana waislamu wawili kwa nyenzo yoyote miongoni mwa nyenzo za kuuwana, mmoja akamuunza mwenzake, basi muuwaji na muuliwaji wote motoni, na kutajwa panga katika hadithi ni sehemu ya mfano tu.