Walilalamikia baadhi ya mafukara wa kiswahaba hali ya umasikini wao kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kutotoa kwao sadaka kwa mali ili wapate malipo mengi kama walivyoyapata ndugu zao wenye mali nyingi na ili na wao wafanye kheri kama wao; kiasi ambacho wao wanaswali kama tunavyoswali, na wanafunga kama tunavyofunga, na wanatoa sadaka kwa mali yao ya ziada na sisi hatutoi! Mtume rehema na amani ziwe juu yake akawaelekeza katika yale wanayoyaweza katika sadaka, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kwani hakukujaalieni Mwenyezi Mungu vile mnavyoweza kuvitoa sadaka kwa ajili nafsi zenu?! Kwani kauli yenu: "Sub-haanallaah" Inakuwa kwenu na malipo ya sadaka, na vile vile kauli: "Allaahu Akbar" ni sadaka, na kauli: "Alhamdulillaah" ni sadaka, na kauli: Laa ilaaha illa llaah" ni sadaka, na kuamrisha mema" ni sadaka, na "kukataza maovu" ni sadaka, bali hata katika tendo la ndoa la mmoja wenu kwa mke wake ni sadaka. Wakashangaa, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hivi akidhi mmoja wenu matamanio yake na awe na malipo katika hilo?! Akasema: Hivi mwaonaje kama akiweka katika haramu kama zinaa au kinginecho, je, atakuwa na madhambi? Hivyo hivyo akiweka katika halali anakuwa na malipo.