Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa katika kila siku inayochomozewa na Jua ndani yake kuna Malaika wawili wanateremka na kunadi, anasema mmoja wao: Ewe Mwenyezi Mungu mpe mwenye kutoa katika njia za utiifu na kwa familia na kwa wageni na sadaka za hiyari mrejeshee na mpe badala bora kuliko kile alichotoa, na umbariki. Na anasema mwingine: Ewe Mwenyezi Mungu mpe bahili mzuiaji uharibifu katika mali yake na uiteketeze mali yake anayoizuia na kutompa mwenye kustahiki.