Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayesema: "Laa ilaaha illa llaahu wahdahu Laa shariika lahu, Lahul-Mulku walahul hamdu Wahuwa a'laa kulli shai-in qadiir", na maana yake nikuwa: Hakuna anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah peke yake asiye na mshirika, nakuwa Yeye Mtukufu amepwekeka kwa Ufalme uliotimia, na mwenye kustahiki kutajwa na sifa na mapenzi na kutukuzwa pasina mwingine asiyekuwa Yeye, nakuwa Yeye ni muweza hakuna chochote kinachomshinda. Atakayeirejea rejea dhikiri hii tukufu kwa siku mara kumi (10); Basi atakuwa kapata malipo mfano wa malipo ya atakayeondoa utumwa kwa watumwa wanne katika watoto wa Ismail bin Ibrahim -Amani iwe juu yao-, na ametaja kizazi cha Ismail -Amani iwe juu yake-; kwa sababu wao ndio watukufu zaidi kuliko wengine.