Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa alikutana na Ibrahim mwandani amani iwe juu yake usiku aliposafirishwa kwenda mbinguni (Israa wal Miiraji), akasema kumwambia: Ewe Muhammadi: Wafikishie umma wako kutoka kwangu salamu, na ulijulishe kuwa Pepo ina udongo mzuri, ina maji matam yasiyokuwa na chumvi, na kuwa Pepo ni pana, ni tambarare haina miti, na kuipanda kwake ni kwa maneno mazuri, nayo ni mema yenye kubakia: Sub-haanallaah, Alhamdulillaah, wa Laa ilaaha illa llaah, wallaahu Akbaru, kila anapoyasema muislamu na kuyarudiarudia hupandia mmea Peponi.