Waislamu walikuwa wakitoa zakatul-fitiri katika zama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake na zama za makhalifa waongofu baada yake kwa mdogo na mkubwa, kiwango cha kibaba cha chakula. Na chakula chao kilikuwa ni ngano na (Zabibu): Zabibu kavu, na (samli): Maziwa yaliyokaushwa na tende. Na kiwango cha kibaba kimoja ni 'mudi' nne, na mudi moja inalingana na ujazo wa viganja viwili vya mtu aliyelingana sawa. Alipokuja Muawia radhi za Allah ziwe juu yake katika mji wa Madina akiwa Khalifa, na ngano ya Sham ilikuwa nyingi wakati huo, alitoa hotuba akasema: Hakika mimi ninaona vibaba viwili vya ngano ya Sham (ni nusu ya kibaba), vinalingana na nusu ya kibaba cha tende, watu wakalichukua hilo. Akasema Abuu Saidi Al-Khudri radhi za Allah ziwe juu yake: Ama mimi ninaendelea kutoa kama nilivyokuwa nikitoa katika zama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake daima maishani mwangu.