Amewajibisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake zakatul-fitiri baada ya Ramadhani, nayo kwa kiwango cha kibaba inafikia uzito wake machoto manne. Na mudi moja: Ni ujazo wa viganja viwili vya mtu wa kati na kati, wa tende au ngano, kwa kila muislamu; aliye huru na mtumwa, mwanaume na mwanamke, mdogo na mkubwa, na hii ni kwa yule ambaye anachakula kinachozidi kwa siku yake hiyo na usiku wake, kwake yeye na kwa wale anaowahudumia. Na akaamrisha itolewe kabla ya watu kutoka kwenda katika swala ya Iddi.