Othman -Radhi za Allah ziwe juu yake- alifundisha sifa ya udhu wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa njia ya vitendo; Ili ueleweka vizuri zaidi, akaomba maji katika chombo, akamimina katika mikono yake mara tatu, na baada ya hapo aliingiza mkono wake wa kulia katika chombo, na akachukua maji akayazungusha kinywani mwake na akayatoa, kisha akavuta kwa pumzi yake kuja ndani ya pua yake, kisha akayatoa na akayapenga, kisha akaosha uso wake mara tatu, kisha akaosha mikono yake pamoja na viwiko viwili mara tatu, kisha akapitisha mkono wake juu ya kichwa chake ukiwa umeloa kwa maji mara moja, kisha akaosha miguu yake pamoja na fundo mbili mara tatu. Alipomaliza radhi za Allah ziwe juu yake akawaeleza kuwa yeye alimuona Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akitawadha mfano wa udhu huu, na akawapa bishara -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa atakayetawadha mfano wa udhu wake, na akaswali rakaa mbili, kwa utulivu na kuhudhuriasha moyo mbele ya Mola wake Mtukufu ndani yake, basi Allah atamlipa kwa udhu huu mkamilifu na kwa swala hii iliyotakaswa kwa kumsamehe yaliyotangulia katika madhambi yake.