Amebainisha Abdallah Bin Zaidi radhi za Allah ziwe juu yake namna ya udhu wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, kwa vitendo, akaomba chombo kidogo chenye maji, kwanza kabisa akaanza kuosha viganja vyake, kisha akainamisha chombo na akamimina maji akaiosha mara tatu nje ya chombo, Kisha akaingiza mikono yake ndani ya chombo, akachota michoto mitatu, katika kila mchoto anasukutua na anapandisha maji puani na anapenga, Kisha akachota kutoka ndani ya chombo akaosha uso wake mara tatu, kisha akachota kutoka ndani ya chombo akaosha mikono yake mpaka katika viwiko viwili mara mbili mbili, kisha akaingiza mikono yake ndani ya chombo akafuta kichwa chake kwa mikono yake akaanza na mbele ya kichwa chake mpaka akafika katika kisogo chake juu ya shingo, kisha akairejesha mpaka akafika mahali alipoanzia, kisha akaosha miguu yake pamoja na kongo mbili.