explain-icon

Ufafanuzi

Anamuhimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kuamka kutoka usingizini mwake kuwa apandishe maji puani na kuyapenga mara tatu; ambako ni kuyatoa maji puani baada ya kuyaingiza, na hii ni kwa sababu Shetani hulala ndani ya tundu za pua - nayo ni pua yote -.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Anaweka sheria kwa kila mwenye kuamka kutoka usingizini apenge ili kuondoa athari za Shetani puani mwake, na endapo kama atatawadha, hapo amri ya kupenga itakuwa ni lazima.
  • Kupenga ni katika faida kamili ya kupandisha maji puani; na kupenga kunatoa uchafu huo kupitia maji.
  • Kufungamanisha na usingizi wa usiku pekee, kwa kuchukua kutoka katika tamko "Kulala" kwani kulala huwa hakuwi ila kwa usingizi wa usiku, kwa sababu ndio usingizi wa kulala muda mrefu na wa fofofo.
  • Katika hadithi kuna dalili kuwa Shetani humgusa mwanadam pasina yeye kulihisi hilo.