Ame apa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ya kuwa vyombo vya Birika lake siku ya kiyama, ni vingi kuliko nyota angani, na kuliko sayari za mbinguni, Na hilo litadhihiri katika usiku wenye kiza ambao hauna mwezi, kwa sababu usiku wenye kuangaza huwa hakuna ndani yake nyota zenye kuonekana kwa kujificha kwake kutokana na mwanga wa mwezi, ambao hauna mawingu, kwa sababu kuwepo kwa mawingu kunazuia kuonekana kwa nyota, Na kwa hakika vyombo vya peponi atakaye kunywa miongoni mwa vinywaji vilivyomo humo, inakuwa ndiyo mwisho kabisa kwa mnywaji kupata kinywaji kwa sababu ya kiu, Na Birika lake linachuruzisha kupitia mabomba mawili yatokayo peponi, na upana wake ni sawa na urefu wake; Hivyo Birika nguzo zake zote zipo sawa, urefu wake ni sawa na umbali ambao upo kati ya Amman mji ambao upo Sham mpaka Aila nao ni mji maarufu uliopo pembeni mwa mji wa Sham, Na maji ya Birika ni meupe sana kuliko maziwa, na ladha yake ni tamu zaidi kuliko Asali.