explain-icon

Ufafanuzi

Ameamrisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kushikamana na Qur'ani na kudumu na kuisoma ili mtu asiisahau baada yakuwa kaihifadhi katika kifua chake, na akalisisitiza hilo kwa kiapo chake -Rehema na amani ziwe juu yake- yakwamba Qur'ani hujitoa haraka mno na kuondoka kutoka vifuani kuliko hata Ngamia aliyefungwa, naye ni yule aliyekazwa kwa kamba kati kati ya muhundi, mtu akikaa karibu naye atamshika, na akimuacha ataondoka na atapotea.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Aliyehifadhi Qur'ani akidumu katika kuisoma kila mara itabakia kuwa imehifadhiwa katika moyo wake, na asipofanya hivyo itaondoka na ataisahau.
  • Katika faida za kushikana na Qur'ani ni: Malipo na thawabu, na kunyanyuliwa daraja siku ya Kiyama.