Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwamba anayesoma Qur'ani, akiwa na hifdhi nzuri na mfanisi, na mahiri na hodari kwa kisomo chake, basi huyu ana thawabu Akhera kiasi cha daraja yake kuwa pamoja na Malaika wema na wakarimu, na kwamba anayesoma Qur'ani na huku akipata tabu ndani yake na anasitasita katika kisomo chake; kwa sababu ya udhaifu wa hifudhi yake, lakini pamoja na hivyo bado anashikamana nayo, na kwake bado ni ngumu na nzito basi ana malipo mara mbili; malipo ya kisomo na malipo ya tabu na kusitasita kwake katika kisomo.