explain-icon

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kila muislamu anayesoma herufi moja katika kitabu cha Mwenyezi Mungu basi atapata jema moja kwa herufi hiyo, na huzidishiwa malipo hayo mpaka mara kumi mfano wake. Kisha akaliweka wazi hilo kwa kauli yake: (Sisemi "Alif Laam Miim" ni herufi, lakini Alif ni herufi, na Laam ni herufi, na Miim ni herufi): Inakuwa herufi zote tatu zina thawabu thelathini (30).

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Himizo la kukithirisha kusoma Qur'ani.
  • Msomaji kwa kila herufi anayoisoma kwa kila neno analolisema huzidishwa mara kumi mfano wake.
  • Upana wa rehema za Allah na ukarimu wake kiasi kwamba huzidishwa malipo kwa waja ikiwa ni fadhila na ukarimu toka kwake.
  • Ubora wa Qur'ani juu ya maneno mengine, na kisomo chake kutumika kama ibada; nakuwa hayo ni maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.