explain-icon

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa muislamu bora na aliye na daraja ya juu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu: Ni yule aliyejifunza Qur'ani, kwa kuisoma na kuihifadhi na kuisoma vizuri na kuielewa na kuitafsiri, na akamfundisha mwingine kile alichonacho katika elimu za Qur'ani pamoja na kuifanyia kazi.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Kumebainishwa utukufu wa Qur'ani, nakuwa ndio maneno bora; kwani ni maneno ya Allah.
  • Mwanafunzi bora ni yule anayefundisha wengine, hatosheki kujifunza mwenyewe pekee.
  • Kujifunza Qur'ani na kuifundisha kunakusanya, kuisoma na maana yake na hukumu zake.