explain-icon

Ufafanuzi

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa maneno yanayopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ni manne. Sub-haanallaah: Na hili linamaanisha kumtakasa Mwenyezi Mungu na kila aina ya mapungufu. Na Al-hamdulillaah: Nako ni kumsifu Allah kwa ukamilifu uliotimia pamoja na kumpenda na kumtukuza. Na Laa ilaaha illa llaah: Yaani: Hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Allah. Na Allahu Akbaru: Yaani: Ni Mtukufu mno, na ni Mtakatifu mno kuliko kila kitu. Nakuwa fadhila zake na kupata thawabu zake si lazima kuyapangilia wakati wa kuyatamka.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Wepesi wa sheria, kiasi kwamba haidhuru kwa neno lipi kati ya hayo utaanza nalo.