explain-icon

Ufafanuzi

Anatueleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa dhikiri bora ni: "Laa ilaaha illa llaah" Na maana yake, hakuna apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa dua bora ni "Al-hamdulillaah"; Nayo inamaanisha kukiri kuwa mneemeshaji ni Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka-, mwenye kustahiki sifa nzuri zilizokamilika.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Himizo la kukithirisha kumtaja Allah kwa neno la tauhidi (Laa ilaaha illa llaah), na kuomba kupitia himidi (Shukurani kwa Allah).