Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayesema: "Nimemridhia Mwenyezi Mungu kuwa Mola" na Mungu na Mlezi na Mmiliki, na bwana na Mtengenezaji, "na Uislamu" kwa hukumu zake zote kwanzia amri zake na makatazo yake "kuwa Dini" mila na sheria, itikadi na utii, "na Muhammadi kuwa Mtume" na Nabii; kwa yote aliyotumwa kwayo na akatufikishia, isipokuwa itamstahikia kwake Pepo.