Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kumtaja Allah Mtukufu kwa maneno haya matukufu ni bora kuliko dunia na vilivyomo, na utajo huo ni kusema: "Sub-haana llaah": Ni kumtakasa Mwenyezi Mungu kutokana na mapungufu. "Alhamdulillaah": Ni kumsifia kwa sifa za ukamilifu pamoja na kumpenda na kumtukuza. "Laa ilaaha illa llaah": Hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu. "Allaahu Akbaru: Mkubwa na Mtukufu kuliko kila kitu.