explain-icon

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-kuhusu maneno mawili anayoyatamka mwanadamu bila uzito wowote na kwa hali yoyote, nakuwa maneno hayo malipo yake ni makubwa katika mizani, nakuwa Mola wetu Mlezi Mwingi wa rehema -Aliyetakasika na kutukuka- anayapenda: Sub-haanallahil Adhwiim, Sub-haanallahi wabihamdihi; Kwakuwa yamekusanya sifa miongoni mwa sifa za Allah kumsifu kwa Utukufu na ukamilifu, na kumtakasa kutokana na mapungufu -Aliyetakasika na kutukuka-.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Dhikri tukufu zaidi ni ile inayokusanya kati ya kumtakasa Allah pamoja na kumtukuza.
  • Kumebainishwa upana wa rehama ya Allah kwa waja wake, kwani Yeye analipa kwa amali ndogo thawabu nyingi.