Amekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake atakayekula kitunguu saumu au kitunguu maji asije msikitini, ili asiwaudhi ndugu zake katika wale wanaohudhuria swala ya jamaa kwa harufu yake, nalo ni katazo la kiusafi la kutokuja msikitini, na si katazo la kula; kwa sababu ni katika vyakula vya halali, na aliletewa Mtume rehema na amani ziwe juu yake chungu kikiwa na mbogamboga, aliponusa ndani yake harufu au alipoambiwa kilichomo, alikataa kula, na akakisogeza kwa baadhi ya Maswahaba zake akasema: Kula; kwani mimi husema na Malaika kwa wahyi. Na akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Malaika hukereka na harufu mbaya, kama wanavyokereka watu kwa harufu hiyo.