explain-icon

Ufafanuzi

Amekataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- muislamu kumhama ndugu yake muislamu zaidi ya siku tatu, wanakutana wote hamsalimii wala hamsemeshi. Na mbora kati ya hawa wagomvi wawili ni yule anayejaribu kuondoa kuhamana huku, na akaanza kwa salamu, na makusudio ya kuhamana hapa ni sababu ya kujikweza, ama kuhamana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kama kuwahama waovu na wazushi na marafiki waovu, hili halina muda maalum, bali limeambatana na masilahi katika kuhama, na linamalizika kwa kuondoka maslilahi yake.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Uhalali wa kumhama mtu ndani ya siku tatu kurudi chini, kwa kulinda maumbile ya kibinadamu, itasamehewa ndani ya siku tatu, ili kiondoke kile kilichojitokeza baina yao.
  • Ubora wa salamu, nakuwa huondoa yaliyoko ndani ya nafsi, nakuwa ni alama ya kupendana.
  • Pupa ya Uislamu juu ya udugu na ukaribu baina waislamu.