explain-icon

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa swala tano za faradhi za usiku na mchana, na swala ya ijumaa kila wiki, na funga ya Ramadhani kila mwaka, vyote hivi hufuta madhambi madogo madogo yaliyo kati yake, kwa sharti la kuyaepuka madhambi makubwa, Ama madhambi makubwa kama zinaa na kunywa pombe haya hayafutwi isipokuwa kwa toba.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Madhambi yako madogo madogo na yako makubwa.
  • Kufutiwa madhambi madogo madogo kumewekwa sharti la ya kuyaepuka makubwa.
  • Madhambi makubwa ni yale iliyokuja adhabu ndani yake katika dunia, au yaliyotajwa kuwa na ahadi ya adhabu huko Akhera; au Makasiriko, au kukawa na kemeo ndani yake, au kulaaniwa mfanyaji wake, kama zinaa na unywaji pombe.