explain-icon

Ufafanuzi

Akasema mtu mmoja katika Masahaba: Laiti ningeliswali nikastarehe, waliokuwa naye waka kana kwamba wamemuabisha kwa hilo, akasema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: Ewe Bilali! Nyanyua adhana na simamisha swala; ilitustarehe kwayo; na hii ni kwa sababu ndani yake kuna kuzungumza na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na raha ya roho na moyo.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Raha ya moyo iko ndani ya swala; kwani ndani yake kuna kuzungumza na Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  • Kemeo kwa mvivu katika ibada.
  • Atakayetekeleza wajibu ulio juu yake, na akajiweka mbali na dhima, atapata raha kwa ibada hiyo na atahisi utulivu.