Ameeleza Anasi bin Maliki radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kuwa miongoni mwa mambo aliyoyakubali Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika sunna zake, ni Muadhini kusema katika Adhana Alfajiri pekee, baada ya kauli yake: "Hayya a'lal falaah" asema: "Asswalaatu khairuni minan nauum" Yaani swala ni bora kuliko usingizi.