Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakuwa yeye alimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hebu nielezeni lau kama Mto ungelikua mlangoni kwa mmoja wenu akioga humo kila siku mara tano, unasemaje kuhusu hilo, kunaweza kubaki na uchafu katika mwili wake?" Wakasema: Hautobakiza uchafu wowote, akasema: " Huu ndio mfano wa swala tano, Mwenyezi Mungu hufuta makosa kwa swala hizo". Sahihi - Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake