explain-icon

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa hatoingia motoni mtu yeyote aliyeswali swala ya Alfajiri, na swala ya Lasiri, na akadumu nazo; na amezitaja maalumu swala hizi mbili; kwa sababu ndizo swala nzito zaidi, na kwa sababu wakati wa Alfajiri huwa ni wakati wa usingizi na ladha yake, na wakati wa Lasiri huwa ni wakati wa kushughulishwa na kazi za mchana na biashara zake, na atakayezihifadhi swala hizi mbili pamoja na kupatikana tabu ndani yake, basi bila shaka ataweza kuzihifadhi swala zingine zilizobakia.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Ubora wa swala mbili, Alfajiri na Lasiri, ni lazima kuzihifadhi.
  • Na atakayezitekeleza swala hizi mara nyingi nafsi yake huepukana na uvivu na kujionyesha na hupenda ibada.