Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mwenye kusali Al-Fajiri basi huwa katika hifadhi ya Mwenyezi Mungu na ulinzi wake na himaya yake, akimtetea, na akimnusuru. Kisha akatahadharisha -Rehema na amani ziwe juu yake- kutoivunja ahadi hii na kuiharibu, ima kwa kuiacha swala ya Al-fajiri, au kumkwaza mwenye kuisali na kumfanyia uadui, kwani mwenye kufanya hivyo atakuwa kauharibu ujirani huu, na atakuwa amestahiki ahadi hii kali, kwa Mwenyezi Mungu kumchunguza yale aliyoyapuuza katika haki zake, na mwenye kuchunguzwa na Mwenyezi Mungu humtia hatiani, kisha humtupa kwa uso wake katika moto.