Anaweka wazi Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake kuwa yeyote atakayeswali swala tano zilizofaradhishwa na wala hakuzidisha zaidi ya hizo swala tano kwa kuswali swala za Sunna, na akafunga mwezi mtukufu wa Ramadhani na akawacha kufunga funga za sunna, na akaamini uhalali wa vilivyo halali na akavitekeleza na akaamini uharamu wa vilivyo haramu na akajiepusha navyo, kwa hakika mtu huyo ataingia Peponi.