Aliingia Ammari bin Yasiri radhi za Allah ziwe juu yake Msikitini akaswali swala ya sunna, na ilikuwa swala fupi sana, alipotoka msikitini, Abdallah ibin Anama alimfuata na akasema kumwambia: Ewe baba Yakdhani, nimekuona umefupisha swala yako!. Akasema Ammari: Je, umeniona nimepunguza chochote katika nguzo zake na wajibu wake na sharti zake?! Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: Hakika mja anaweza kuswali swala, na asiandikiwe malipo yoyote isipokuwa moja yake ya kumi, au tisa ya kumi, au nane ya kumi, au saba ya kumi, au sudusi yake, au tano ya kumi, au robo yake, au theluthi yake, au nusu yake.