explain-icon

Ufafanuzi

Amekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kujitengenezea makonde na mabustani na mashamba; kwa sababu hilo ni katika sababu za kuipenda sana dunia na kubweteka nayo na kuisahau Akhera.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Katazo la kukithirisha sana hadhi za kidunia kwa sababu hupelekea kuiacha Akhera.
  • Katika hadithi hakuna katazo la kutengeneza yale yanayopelekea maisha, bali katazo ni kuzama katika dunia na kuisahau Akhera.
  • Amesema Sanadi: Na makusudio yake: Nikuwa msizame katika kutengeneza mabustani, mkapumbazika nayo na mkajisahau kumtaja Mwenyezi Mungu.