explain-icon

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba hakuna maisha halisi isipokuwa maisha ya Akhera katika radhi za Mwenyezi Mungu na rehema zake na pepo yake; kwa sababu maisha ya Dunia huondoka, na maisha ya Akhera ndio ya kudumu na kubakia, kisha akawaombea msamaha na ukarimu na kutengemaa rehema na amani ziwe juu yake Maanswari wale waliompa makazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake pamoja Muhajirina wale walioacha miji yao na mali zao wakitafuta fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu na radhi zake.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Kutoipenda kwake Dunia rehema na amani ziwe juu yake na kuilekea kwake Akhera.
  • Kuuepushia Mtume rehema na amani ziwe juu yake umma wake na kupenda starehe za Dunia zenye kuondoka.
  • Kumebainishwa nafasi ya Muhajirina na Answari, kiasi kwamba walibahatika kupata dua ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kuwaombea msamaha.
  • Mja hafurahii yale anayoyapata katika Dunia kwani huondoka upesi pamoja nakuwa na mateso makubwa, bali nyumba ya makazi ya kudumu ni Akhera.