explain-icon

Ufafanuzi

Amehimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake juu ya kukithirisha kukikumbuka kifo ambacho kukikumbuka kwake mtu anakumbuka Akhera, na kunabomoa mapenzi yake ya kupenda ladha za dunia ndani ya moyo wake, na hasa hasa zile za haramu.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Kifo kinakata ladha za dunia, lakini kwa muumini kinamuhamisha kwenda katika ladha za Akhera na ladha za pepo na yale yanayopatikana ndani yake miongoni mwa kheri kubwa.
  • Kukumbuka kifo na yale yanayokuwa baada yake ni miongoni mwa sababu za kutubia na kujiondoa katika dhambi na kujiandaa na Akhera.