explain-icon

Ufafanuzi

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba amefaulu na amebahatika atakayemtii Mola wake akaongozwa na akawezeshwa kuingia katika Uislamu, na akaruzukiwa katika halali kiasi cha mahitaji yake pasina ziada wala mapungufu, na Mwenyezi Mungu akamjaalia kukinai na kuridhika na kile alichompa.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Utukufu wa mtu upo katika ukamilifu wa dini yake na kupata cha kumtosheleza katika maisha yake na kutosheka kwake na kile alichopewa na Mwenyezi Mungu.
  • Himizo la kutosheka kwa kile ulichopewa katika dunia ikiwa ni pamoja na Uislamu na sunna.