Maswahaba walimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Hivi je mnata nikuelezeni na nikufundisheni amali bora zaidi kuliko zote katika amali zenu, na yenye utukufu kuliko zote na yenye kukua zaidi na safi zaidi na takatifu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu Mfalme Aliyetukuka? na yenye nafasi ya juu zaidi katika nafasi zenu za peponi? na ambayo ni bora zaidi kwenu kuliko kutoa sadaka ya Dhahabu na fedha? na bora kwenu kuliko hata kukutana na makafiri vitani, mkapiga shingo zao, na wakapiga shingo zenu? Maswahaba wakasema: Ndio tunalitaka hilo. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Ni kumtaja Mwenyezi Mungu katika nyakati zote na katika mikao yote na hali zote.