Ameeleza Nuuma bin Bashiri radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, ya kwamba mama yake Amra binti Rawaha radhi za Allah ziwe juu yake alimuuliza baba yake baadhi ya zawadi katika mali yake kwa mwanaye, akawa mzito, na akachelewa kumjibu kwa muda wa mwaka mzima, kisha akaona amjibu swali lake, akamhofia mwanaye Nuuman, akasema: Siridhii mpaka umfanye kuwa shahidi Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa kile ulichomzawadia mwanangu, baba yangu akanishika mkono na mimi wakati huo nikiwa kijana mdogo, akumuendea Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika mama wa kijana huyu, binti Rawaha kapendezwa nikufanye kuwa shahidi kwa kile nilichomzawadia mwanaye, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Ewe Bashiri, je, una mtoto mwingine asiyekuwa huyu? Akasema: Ndiyo. Akasema: Je, wote umewazawadia mfano wa huyu. Akasema: Hapana. Akasema: Basi usinifanye mimi kuwa shahidi, kwani mimi sishuhudii upendeleo na dhulma. Na kwa Muslim alisema kwa kumkemea: Lakini mshuhudishe katika dhulma hii mwingine asiyekuwa mimi.