Jabiri bin Abdillah Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili, alimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema katika mwaka wa ufunguzi akiwa Makka: Hakika Mwenyezi Mungu na Mtume wake amekataza kuuza pombe, na mzoga na nguruwe na masanamu, wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, je inajuzu kwetu kuuza mafuta ya wanyama waliokufa? Kwa sababu yanatumika kupaka boti (Mitumbwi), na ngozi na watu huwasha taa zao kwayo. Akasema: Hapana, kuyauza ni haramu, kisha akasema: Mwenyezi Mungu amewalaani Mayahudi, Mwenyezi Mungu alipowaharamishia mafuta ya wanyama, waliyayeyusha, kisha wakayauza na kula thamani yake.