explain-icon

Ufafanuzi

Alikataza Mtume -rehema na amani ziwe juu yake kula kila chenye kuwinda katika wanyama wenye kushambulia, kinachowinda kwa meno ya mbele, na akakataza kula kila ndege anayekata na kukamata kwa mdomo wake.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Pupa ya Uislamu juu ya vitu vizuri katika kila kitu miongoni mwa vyakula na vinywaji na vinginevyo.
  • Asili katika vyakula ni uhalali; isipokuwa vile vilivyoelezwa na sheria kuwa ni haram.