Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kitakapotatiza chochote tumboni kwa mwenye kusali, akapata shaka, je kuna chochote kimemtoka au la?, asiondoke katika swala yake na akaikatisha kwa ajili ya kurudia udhu, mpaka apate uhakika wa kutenguka udhu wake; ima kwa kusikia sauti ya upepo, au anuse harufu; kwa sababu mwenye uhakika habatilishi uhakika wake kwa shaka, hali yakuwa ana uhakika na twahara, na hadathi (kutengukwa udhu) kunatiliwa shaka.