explain-icon

Ufafanuzi

Amebainisha Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kuwa ni lazima kuzuia madhara kwa aina zake zote na sababu zake zote kwako na kwa wengine, ni haramu kwa yeyote kujiudhi mwenyewe na mwingine kwa kiwango sawa. Na ni haramu kwake kukabiliana na madhara kwa madhara; kwa sababu madhara hayaondoshwi kwa madhara, isipokuwa kama itakua katika njia ya kulipiza kisasi pasina kuvuka mipaka.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Katazo la kulipiza kwa zaidi ya vile ulivyofanyiwa.
  • Mwenyezi Mungu hakuwaamrisha waja wake lolote lenye kuwadhuru.
  • Hadithi ni kanuni katika kuharamisha kujidhuru, na kudhuru kwa kauli au vitendo au kuacha.
  • Katika kanuni za sheria: Ni "Madhara huondoshwa", Hivyo, sheria haikubaliani na madhara, na inakataza kujidhuru.