explain-icon

Ufafanuzi

Ameeleza Ally bin Abiy Twalib Radhi za Allah ziwe juu yake yakuwa yeye ilikuwa mara nyingi akitokwa na madhii -nayo ni maji meupe mepesi yenye utelezi hutoka katika tupu wakati wa matamanio au kabla ya tendo ya ndoa-, Na wala hajui afanye nini yakitoka, akaona haya kumuuliza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake; kwa sababu yeye ni mume wa Fatma binti wa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake, Akamuomba Mikidadi bin Aswadi amuulize Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kuhuus hilo, Basi akajibu Mtume Rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa aoshe tupu yake kisha atawadhe.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Ubora wa Ally bin Abi Twalib Radhi za Allah ziwe juu yake, kiasi ambacho haya haikumzuia kuacha kuuliza kupitia mtu mwingine.
  • Inafaa kutuma mtu kwa niaba kwa ajili ya kuuliza.
  • Inafaa kumueleza mtu mambo binafsi kwa sababu ya kuona haya ikiwa kuna masilahi.
  • Unajisi wa madhii, na uwajibu wa kuyaosha katika mwili na nguo.
  • Kutoka kwa madhii ni katika vitenguzi vya udhu.
  • Uwajibu wa kuosha utupu na korodani mbili kwa kuwa zimetajwa katika hadithi nyingine.