explain-icon

Ufafanuzi

Anaeleza Anasi bin Maliki radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba alikuwa yeye pamoja na mtumishi mwenye kukaribiana naye katika umri wake, wakimfuata Mtume rehema na amani ziwe juu yake pindi anapotoka kwenda kikidhi haja yake, walikuwa wakibeba fimbo yenye meno (mkongojo) mfano wa meno ya mshale ili aifanye kuwa sitara ya kutundukia kitu chenye kusitiri, au sitara kwa ajili ya swala yake, na walikuwa wakibeba pia chombo kidogo cha ngozi kilichojaa maji , anapomaliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kukidhi haja yake, basi mmoja wao anampa chombo, basi anastanji kwa maji.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Muislamu anatakiwa kujiandaa kwa maji (au chochote cha kujisafishia) wakati wa kukidhi haja; ili asijekuhitaji kusimama akajichafua.
  • Kuhifadhi uchi wakati wa kukidhi haja asijekumtazama yeyote; kwa sababu kutazama katika uchi ni haramu, kwani alikuwa kichomeka fimbo katika Ardhi na akifunga nguo yenye kusitiri.
  • Kuna haja kubwa ya kuwafundisha watoto adabu za kiislamu na kuwalea katika adabu hizo; ili warithishane.