Alikutana Mtume rehema na amani ziwe juu yake na Abuu Huraira radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake katika baadhi ya njia za Madina, na Abuu Huraira alikuwa na janaba, na kwa sababu ya kumuheshimu kwake Mtume rehema na amani ziwe juu yake alichukia kukaa naye na kuzungumza naye hali yakuwa yuko katika hali ile, kwa kudhani kwake kuwa yeye ni najisi, akaenda kwa uficho na akaoga, kisha akarejea na akakaa, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamuuliza kuwa alikwenda wapi? Akamueleza kuhusu hali yake, na kwamba yeye alichukia kukaa naye hali yakuwa yeye ni najisi kwa sababu ya janaba, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akastaajabu, na akasema: Hakika muumini ni msafi na wala hanajisiki kwa hali yoyote; akiwa hai na hata wakiwa maiti.