Alikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake anapotaka kuoga janaba anaanza kwa kuosha mikono yake, kisha anatawadha kama anavyotawadha udhu wa swala, kisha anajimwagia maji katika mwili wake kisha anaachanisha nywele za kichwa chake kwa mikono yake, mpaka anapohisi kuwa maji yamefika katika maoteo ya nywele zake, na yameloanisha ngozi, anajimwagia maji kichwani mara tatu kisha anaosha mwili mzima. Na akasema Aisha Radhi za Allah ziwe juu yake: Nilikuwa nikioga mimi pamoja na Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kutoka katika chombo kimoja, tukichota sote.