explain-icon

Ufafanuzi

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake baadhi ya adabu: Akakataza kwa mwanaume kushika uume wake kwa mkono wa kulia wakati wa kukidhi haja, na kuondoa uchafu katika utupu wa mbele au wa nyuma kwa mkono wa kulia, kwa sababu mkono wa kulia umetayarishwa kwa matendo mema, Kama ambavyo alikataza mtu kupumulia ndani ya chombo anachonywea ndani yake.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Hii inaweka wazi namna ambavyo Uislamu umetangulia kuleta ustaarabu katika adabu na usafi kabla ya watu wengine.
  • Kuepuka mambo machafu, ikiwa hakuna budi basi afanye kwa mkono wa kushoto.
  • Kumebainishwa utukufu wa mkono wa kulia, na ubora wake juu ya mkono wa kushoto.
  • Ukamilifu wa sheria ya Uislamu na kuenea mafundisho yake kila nyanja.