Kutoka kwa Wahshiy bin Harbi radhi za Allah ziwe juu yake: Ya kwamba wao walisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika sisi tunakula lakini hatushibi, akasema: "Huenda nyinyi mnakula kila mtu peke yake?" Wakasema: Ndiyo. Akasema: "Basi kusanyikeni katika chakula chenu, na mkitajie jina la Mwenyezi Mungu, mtabarikiwa katika chakula hicho". Ni nzuri (Hasan) - Imepokelewa na Abu Daud, Ibn Majah na Ahmad
explain-icon

Ufafanuzi

Baadhi ya Maswahaba walimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake, wakasema: Hakika sisi tunakula lakini hatushibi. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kuwaambia: Huenda nyinyi kila mtu hukaa peke yake wakati wa kula; akala kila mtu peke yake? Wakasema: Ndiyo. Akasema: Basi kusanyikeni na mle pasina kutengana, na mtaje jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kula kwa kusema: Bismillaah, (kwa jina la Mwenyezi Mungu) mtabarikiwa ndani yake na mtashiba.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Kukusanyika kwa ajili ya chakula na kutaja jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kula ni sababu ya kupata baraka katika chakula, na kupatikana shibe kwa kukila kwake.
  • Utengano wote ni shari, na umoja wote ni heri.
  • Himizo la kukusanyika na kutaja jina la Mwenyezi Mungu wakati wa chakula.
  • Amesema Assanadi: Kwa sababu ya mkusanyika baraka huteremka katika chakula, na kwa kulitaja jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu Shetani hushindwa kukifikia chakula.